Tangazo!!

WARSHA YA UANDISHI WA MISWAADA YA FILAMU/SCREENPLAY WORKSHOP(Level 1)
Je ?unajua kuwa hadithi za Filamu zozote hujengwa kwa wahusika, wahusika ndiyo wabeba lengo zima la filamu? je wajua jinsi ya kuwajenga wahusika wako ili waweze kubeba lengo la hadithi ya Filamu  kiufasaha? je unajua kuwa ukikosea kumjenga mhusika mkuu katika hadithi ya Filamu  yako ni vigumu hadithi ya Filamu bora? basi ukitaka kuyajua yote haya karibu katika warsha ya uandishi wa miswada ya filamu pale IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kuanzia tarehe 13-15 Februari 2012 ,Kutakuwa na Warsha ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu/Screenplay Workshop(Level 1) , Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana , Cheti cha Ushiriki kitatolewa mwishoni mwa mafunzo.
 Warsha itakuwa kwa Kiswahili (na Kiingereza ikibidi) na mshiriki anaweza kuwa mtu yoyote anayependa kuandika miswada ya filamu (amateur scriptwriter) au mwandishi anayechipukia (upcoming scriptwriter)
Hima wadau wote wa Tasnia ya Filamu ,Sanaa, Sanaa za Maonyesho na Uandishi wa ubunifu msikose nafasi hii muhimu ya warsha mafunzo daraja la kwanza ilikujijengea misingi mizuri ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na warsha hii tafadhali wasiliana na IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ,Ndg.John Mwakilama Simu Namba 0714 13 22 49,  na barua pepe :mwakilamajohn@yahoo.com