Wednesday, June 20, 2012

Wakazi wa Ubungo mpo tayari?????????????????? njoo upate mwangaza juu ya katiba ya nchi yetu iliyopo ili uwezeshiriki kikamilifu katika marekebisho ya katiba


Alice Foundation inakukaribisha Tarehe 24 juni 2012 katika viwanja vya sanaa sinza legho jijini Dar-es salaam.tutakuwa na  wageni kutoka nchi ya Marekani ambao wataambatana na viongozi kutoka Ubalozi wa Marekani tunatarajia kuwa na ugeni wa watu 100 na wananchi 900 wakazi wa Kata ya  Ubungo, Ubalozi wa Marekani wanatuletea Navy band- bendi ya kikosi cha jeshi la maji, pia watatumia fursa hiyo kutupatia mipira ya kikapu ambayo tulikuwa tumeomba ubalozini hapo mapema mwaka huu.


Pamoja na ugeni huo lengo letu hasa ni kutoa elimu ya Afya na mazingira kwa watoto wanaoishi mazingira magumu na hatarishi pamoja na walezi wao. Hivyo tutakuwa na michezo mbalimbali, na tutakuwa na zoezi la kupima VVU kwa hiari. ambalo  litafanyika bure kwa wananchi wote. Na kufanya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Elimu ya  katiba iliyopo ili wananchi wa kata ya Ubungo  waweze kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni juu ya katiba mpya.